1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahamiaji 16 kutoka Afrika wafa maji wakiwania kuingia Ulaya

7 Agosti 2023

Wahamiaji16 kutoka Afrika wamekufa na makumi wengine hawajulikani waliko baada ya boti walizokuwa wakisafiria kujaribu kuingia Ulaya kuzama kwa nchini Tunisia, Morocco na kwenye kisiwa cha Lampedusa nchini Italia.

https://p.dw.com/p/4Us6M
Tunesische Küstenwache stoppt Schiff mit Migranten auf dem Weg nach Italien
Picha: Hasan Mrad/ZUMA/picture alliance

Nchini Tunisia, mamlaka zimesema jumla wahamiaji 11 wamekufa na wengine 44 wamepotea baharini katika ajali ya kuzama kwa boti iliyotokea mwishoni mwa juma kwenye mji wa mwambao wa bahari ya Mediterrania wa Sfax.

Kwa upande wake, jeshi la Morocco limearifu kuwa limeopoa miili ya wahamiaji 5 wote kutoka Senegal na kuwaokoa wengine 189 ambao boti yao ilizama kwenye pwani ya Sahara magharibi. 

Soma zaidi: Wahamiaji 30 kutoka Afrika wapotea baharini

Hayo yameripotiwa wakati mamlaka za Italia bado zinawatafuta wahamiaji wengine 30 waliopotea baada ya boti mbili za wahamiaji kuzama karibu na kisiwa cha Lampedusa. 

Kwa miongo kadhaa, safari za wahamiaji wanaotumia boti za mpira wakijaribu kuvuka bahari ya Atlantiki na ile ya Mediterania kwa lengo la kuingia Ulaya zimegharimu maisha ya maelfu ya watu kaskazini mwa Afrika