1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTaiwan

Wagombea Urais Taiwan wachuana katika mdahalo

30 Desemba 2023

Wagombea urais katika kisiwa kinachojitawala cha Taiwan wamechuana hii leo katika mdahalo wa kuelezea misimamo yao hasa kuhusu uhusiano wa Taiwan na China.

https://p.dw.com/p/4ajJN
Taiwan, Taipeh | Tsai Ing-wen bei Feierlichkeiten zum Nationalfeiertag
Rais wa sasa wa Taiwan Tsai Ing-wen.Picha: Chiang Ying-ying/AP/dpa/picture alliance

Mdahalo huo unajiri karibu wiki mbili kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Januari 13, 2024 na unaofuatiliwa kwa karibu na Washington na Beijing.

Wagombea hao walipambana katika mjadala uliorushwa moja kwa moja kwenye runinga na mgombea wa chama kilichopo madarakani cha Democratic Progressive Party (DPP) ambaye pia ni Makamu wa rais Lai Ching-te, ametetea sera ya chama chake cha ya kutaka uhuru wao kutoka kwa China.

Wapinzani wake walimshambulia mara kwa mara, wakisema kuwa matamshi yake ya kuunga mkono uhuru "yatadhoofisha usalama wa Taiwan".

China inadai kuwa kisiwa cha Taiwan ni sehemu ya himaya yake, na imeapa kutumia mabavu kukidhibiti ikiwa italazimika, na ilisitisha mawasiliano ya ngazi za juu na Rais wa sasa wa Taiwan Tsai Ing-wen.