1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wageni wanaowasili Guinea ya Ikweta kupimwa Ebola

16 Januari 2015

Dimba la Kombe la Mataifa ya Afrika hatimaye limefungua pazia zake leo Jumamosi nchini Guinea ya Ikweta, huku waandalizi wakitumai kuwa yatakuwa mashindano ya kufana

https://p.dw.com/p/1ELlm
Afrika Cupa Angola Fans
Picha: A.Joe!AFP/Getty Images

Hii ni baada ya Morocco kujiondoa kutokana na hofu ya kusambaa ugponjwa w Ebola ambao umewauwa maelfu ya watu katika eneo la Afrika Magharibi.

Serikali ya Guinea ya Ikweta ilichukua hatua za kuzuia Ebola kutua katika ardhi yake, ikiwa ni pamoja na kuwaajiri watalaamu wa matibabu kutoka Cuba, lakini kwa upande wa kandanda, mechi nyingi huenda zikachezwa mbele ya viwanja vitupu katika nchi hiyo yenye idadi ya jumla ya watu 700,000.

Na mojawapo ya hatua za tahadhari zilizochukuliwa, timu zote zinazowasili nchini humo lazima zipitie katika mji mkuu Malabo na kufanyiwa vipimo vya virusi vya Ebola. Kando na timu zinazishiriki, pia wageni wanawasili nchini humo wanafanyiwa vipimo.

Äquatorialguinea Bata Stadion
Uwanja wa michezo wa Bata nchini Guinea ya IkwetaPicha: picture-alliance/dpa/abaca

Shirikisho la Kandanda Afrika CAF limesema watakaopatikana na dalili za kuwa na virusi hivyo hatari, au watakaokataa kufanyiwa vipimo, watawekwa katika karantini kwa hadi siku 21.

Lakini licha ya kuwepo ukosoaji kuhusiana na hofu ya uwezo wan chi hiyo kuandaa dimba hilo katika kipindi kifupi baada ya Morocco kujiondoa, maafisa wa Guinea ya Ikweta wanasisitiza kuwa kila kitu kimekamilika tayari kwa tamasha hilo. Algeria ambayo ndiyo timu inayoongoza barani Afrika katika viwango vya orodha ya FIFA, inaikuta katika moja ya makundi mawili magumu, ambapo Mbweha hao wa jangwani wakipangwa pamoja na Ghana, Senegal na Afrika Kusini katika Kundi C.

Washindi wa kundi hilo wanaweza kujikuta katika mchuano wa robo fainali dhidi ya washindi wa pili wa Kundi D, ambalo lina Cote d'Ivoire, Mali, Cameroon na Guinea. Katika Kundi A lina Congo Brazzaville, Gabon, wenyeji Guinea ya Ikweta na Burkina Faso wakati Kundi B lina Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Tunisa na Cape Verde.

Na katika muda mfupi ujao, wenyeji Guinea ya Ikweta wanafungua dimba dhidi ya Congo Brazzaville na kisha mchuano wa pili utakuwa kti ya Burkina Faso na Gabon. Kesho Jumapili, Zambia watachuana na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wakati Tunisia wakipambana na Cape Verde.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Yusuf Saumu