1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafungwa watoroka gerezani DRC

10 Agosti 2022

Gereza kuu la mji wa kibiashara wa Butembo, katika mkoa wa Kivu ya Kaskazini nchini Congo lilishambukiwa na kundi la kigaidi kutoka Uganda ADF milango ya saa nane alfajiri.

https://p.dw.com/p/4FMVL
Großbritannien Schlüssel zu Nelson Mandelas Gefängniszelle
Picha: JOR/Capital Pictures/picture alliance

Waasi hao waliotokea katika eneo la utawala wa Bashu kaskazini mashariki ya Butembo, walifanya shambulizi lao katikati mwa mji huo na kurudi walikotokea baada ya operesheni yao kufanikiwa. Gereza hilo muhimu la mji huo lilikuwa linawahifadhi wafungwa zaidi ya mia nane na inasemekana kuwa ni zaidi ya wafungwa kumi tu ndio walibaki katika gereza hilo. 

Duru toka vyombo vya usalama zadokeza, kuwa wakati wa shambulizi la leo jumatano alfajiri, askari polisi wawili pamoja na muasi mmoja waliuawa.

Wapiganaji wa Maimai wanatajwa kuhusika na shambulizi la gereza.

Kongo Zaire Kindersoldaten
Baadhi ya wanajeshi wa ButemboPicha: AP

Na kwenye kitangazo chake, msemaji wa jeshi la serikali katika secta ya kijeshi Sokola1 eneo la Kaskazini kubwa la mkoa wa Kivu ya Kaskazini captain Anthony Mualushayi alisema, kwamba ni wapiganaji wa maimai ndio walilishambulia gereza hilo, akiahidi kutoa maelezo zaidi baadae jioni. 

Hata hivyo wakaazi waliowaandama waasi hao ili jeshi lisipoteze nyayo zao,walikuwa wakiwapigia simu viongozi wa jeshi, ili kuwafyeka waasi hao wanaodhaniwa kwamba ni ADF.

Wakizungumza na DW, baadhi ya wakaazi waliowaona ADF hao walisema, kuwa katika kurudi kwao mahali walikotokea walisema, kwamba katika safari yao, waasi hao walikuwa wakipora maduka pamoja na nyumba kadhaa, pale wakiwateka pia raia. 

Hiyo ilikuwa kati ya saa kumi na moja na saa kumi na mbili alfajiri. 

Naye msemaji wa mashirika ya kiraia katika mji wa Butembo Vake Okello alisema, kwamba kushambuliwa kwa gereza kuu la Kakwangura kunawatia hofu wakaazi, na anafofia kuona mji huo unashambuliwa mara tena na ADF.

Vake Okello alitumia fursa hiyo kutoa mwito kwa jeshi la serikali kuimarisha usalama kwenye viunga vya mji wa Butembo, ili kuhakikisha kwamba ADF hawaushambulii tena mji huo. 

Hadi sasa operesheni za kuwaandama waasi hao zinaendelea katika Kongamano la Bashu, na jeshi huenda likatoa taarifa zaidi, hasa matokeo ya operesheni hizo baadae. 

Soma zaidi:Waliouawa kwenye maandamano DRC kuzikwa Ijumaa

Katika shambulizi la leo mjini Butembo, ni watu sita waliuawa,yaani askari polisi wawili, na watu wengine wanne walioshukiwa na raia kwamba ni ADF. 

Watatu kati ya waasi waliouawa na kuchomwa moto na wakaazi wenye hasira, walichomwa moto baada ya kuuawa.

Shambulizi la gereza kuu la Butembo Kakwangura linafanyika miaka miwili,baada ya gereza kuu la Beni Kangwayi kushambuliwa na ADF, kwaajili ya kuwatorosha wapiganaji wao wafungwa.

DW Beni.