1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waandamanaji Pakistan wamtaka jaji mkuu ajiuzulu

15 Mei 2023

Mamia ya waandamanaji wanaoiunga mkono serikali ya Pakistan wanamshinikiza jaji mkuu kujiuzulu kwa kumuachia waziri mkuu wa zamani, Imran Khan, baada ya kukamatwa wiki iliyopita.

https://p.dw.com/p/4RN3g
Pakistan | Protest Islamabad
Picha: Abdul Sattar/DW

Khan, ambaye aliondolewa madarakani mnamo mwezi Aprili mwaka uliopita, alikamatwa siku ya Jumanne kufuatia miezi kadhaa ya mgogoro wa kisiasa, na kusababisha wafuasi wake kuandamana katika miji mbalimbali nchini humo.

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan arejea nyumbani

Hata hivyo, kukamatwa kwake kulitangazwa kuwa ni kinyume cha sheria na jaji mkuu na baadaye mwanasiasa huyo mkongwe aliachiliwa na kupewa kinga ya kutokamatwa.

Kulikuwepo na ulinzi mkali katikati mwa mji mkuu Islamabad wakati waandamanaji walipokusanyika nje ya majengo ya mahakama.