1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafrika Kusini wafukuzwa Zimbabwe

30 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEpV

Harare:

Zimbabwe imewafukuza nchini Marubani wawili wa Afrika Kusini waliokamatwa kwa makosa ya kuwasafirisha mamluki wa njama iliyoshindwa ya kutaka kuipindua serikali ya Guinea ya Ikweta. Watu hao wawili walitaka kufunguliwa leo lakini Wakili wao, Jonathan Samkange, amesema kuwa wameachiliwa jana na kusafirishwa kwa njia ya barabara hadi Afrika Kusini. Marubani hao wamekamatwa mwezi wa Machi mwaka wa jana pamoja na watu wengine 68 wakiwa na pasi za Afrika Kusini baada ya ndege yao kuzuiliwa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Harare. Maafisa wa Zimbabwe wamesema kuwa watu hao walikuwa sehemu ya kikundi kikubwa kilichotaka kuipindua serikali ya Guinea ya Ikweta ambayo ina utajiri mkubwa wa mafuta. Wageni 11 mwezi wa Novemba mwaka wa jana wamehukumiwa vifungo vya miaka 14 mpaka 34 kwa njama za kutaka kuipindua serikali. Marubani hao wamepatikana na hatia ya kuvunja sheria za anga na silaha. Walihukumiwa kifungo cha miezi 16 katika jela ya Chikurubi iliyoko mjini Harare.