1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Wafaransa wajitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi wa Bunge

30 Juni 2024

Wananchi wa Ufaransa wanapiga kura hivi leo katika duru ya kwanza ya uchaguzi Bunge.

https://p.dw.com/p/4hgnK
Wananchi wa Ufaransa wakipiga kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa Bunge
Wananchi wa Ufaransa wakipiga kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa BungePicha: LUDOVIC MARIN/AFP

Uchaguzi huo unaweza kushuhudia chama cha mrengo mkali wa kulia cha Marine Le Pen cha National Rally kikichukua madaraka.

Hii itakuwa hatua ya kihistoria kwa chama cha mrengo mkali wa kulia  kushinda wingi wa viti bungeni na itakuwa kwa mara ya kwanza nchini Ufaransa tangu uvamizi wa Wanazi wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Vituo vya kupigia kura vimefungulia tangu saa mbili asubuhi na vitafungwa saa kumi na mbili jioni.

Rais Emmanuel Macron aliitisha uchaguzi wa mapema baada ya chama chake kupata pigo katika uchaguzi wa Bunge la Ulaya. Wananchi wa Ufaransa wanalalamikia mfumuko wa bei za bidhaa kama chakula na nishati.