1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUjerumani

Wafanyikazi wa Lufthansa waitisha mgomo wa siku tatu

28 Februari 2024

Muungano wa vyama vya wafanyikazi nchini Ujerumani Verdi umeitisha mgomo wa kitaifa wa siku tatu wa wafanyikazi wanaohusika na shughuli za ndani katika shirika la ndege la Lufthansa kuanzia leo hadi siku ya Ijumaa.

https://p.dw.com/p/4cxiO
Ndege za Lufthansa zimeegeshwa katika uwanja wa ndege wa Frankfurt nchini Ujerumani.
Ndege za Lufthansa zimeegeshwa katika uwanja wa ndege wa Frankfurt nchini Ujerumani.Picha: Michael Probst/AP/picture alliance

Muungano wa vyama vya wafanyikazi nchini Ujerumani Verdi umesema safari za ndege za abiria hazitaathirika kutokana na mgomo huo.

Shirika la ndege la Lufthansa limeeleza kuwa linatathmini athari za mgomo huo ambazo huenda zikajitokeza kuanzia leo hadi siku ya Ijumaa.

Wafanyikazi wa Lufthansa tayari wamefanya migomo miwili mwezi huu.

Mgomo wa hivi karibuni ulifanyika Februari 20 na ulihusisha mafundi, wapakiaji mizigo na wafanyikazi wengine wa ndani huku Lufthansa ikilazimika kufuta asilimia 90 ya safari zake za ndege wakati huo.

Verdi inashinikiza nyongeza ya mishahara kwa wafanyikazi wa Lufthansa huku duru ya pili ya mazungumzo kati yao na shirika hilo la ndege ikitarajiwa kufanyika mwezi Machi tarehe 13-14.