1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafadhili watakiwa kuwekeza Afghanistan

8 Julai 2012

Damu na mali vilivyotolewa mhanga katika muda uliopita huenda vikawa vimepotea bure bila kuwapo na uwekezaji nchini Afghanistan wakati majeshi ya kimataifa yatakapoondoka,mkutano wa wafadhili umefahamishwa mjini Tokyo.

https://p.dw.com/p/15TV7
In this Thursday, July 5, 2012 photo, an Afghan laborer carries a stone, as a grader vehicle works on a road to make it ready for asphalt in Kabul, Afghanistan. Afghanistan will seek at least $4 billion from international donors this weekend at a crucial aid conference aimed at propping up the country after most foreign combat troops leave at the end of 2014. (AP Photo/Musadeq Sadeq)
Ujenzi mpya wa kijamii nchini AfghanistanPicha: AP

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon , ambaye ni miongoni mwa viongozi maarufu waliokusanyika katika mji mkuu wa Japan Tokyo kwa ajili ya mazungumzo juu ya kile kinachojulikana kama , "muongo wa mabadiliko" amesema kuwa hatua za maendeleo katika usalama na maendeleo kwa jumla zimepigwa, lakini bado ni tete.

Kushindwa kuwekeza katika serikali , sheria, haki za binadamu, ajira na maendeleo ya jamii kunaweza kurejesha nyuma uwekezaji na hatua za kujitolea muhanga ambazo zimefanyika katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, Ban amewaambia viongozi katika mkutano huo.

United Nations Secretary-General Ban Ki-moon speaks with the media after Security Council consultations at U.N. headquarters in New York June 7, 2012. There is a growing threat of full-scale civil war erupting in Syria, where more than a year of violence between government forces and opposition fighters shows no signs of abating, Ban said on Thursday. REUTERS/Allison Joyce (UNITED STATES - Tags: POLITICS)
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki MoonPicha: Reuters

Mkutano huo una lengo la kupunguza mwanya kati ya kile ambacho serikali mjini Kabul inakipata kutokana na uchumi wake na kile inachohitaji kwa ajili ya maendeleo ya nchi hiyo na kuwa thabiti.

Afghanistan yataka msaada

Rais wa Afghanistan Hamid Karzai, ambaye yuko mjini Tokyo pamoja na waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Hillary Clinton na katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon , ametoa wito wa nchi yake kupatiwa kiasi cha dola bilioni 4 kila mwaka kama msaada wa kijamii.

Siku ya Jumamosi Japan ilitangaza kuwa wafadhili watatoa zaidi ya dola bilioni 16 kama msaada wa kijamii katika muda wa miaka minne hadi mwaka 2015.

Tuko katika wakati mgumu katika historia ya Afghanistan, katika hatua za mpito kutoka utegemezi wa misaada ambayo imesaidia taasisi za nchi hiyo kuota mizizi hadi katika uhusiano wa kawaida wa kitaifa, Afghanistan inayoweza kufanyakazi pamoja na watu wake pamoja na washirika wake wa kimataifa, Ban amesema.

Usalama bado tatizo

Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo , rais wa Afghanistan Hamid Karzai amekiri kuwa usalama unaendelea kuwa tatizo kubwa, lakini ameongeza kuwa nchi yake imetoka mbali hadi ilipo sasa.

Katika miaka kumi iliyopita , kwa msaada kutoka jumuiya ya kimataifa , tumepiga hatua kubwa za kimaendeleo kuelekea kuponesha makovu ya mizozo na uharibifu, amesema.

Tunajenga njia mpya kwa ajili ya watu wetu kufikia yale wanayokusudia ya mafanikio ya amani pamoja na kuwa na nchi yenye demokrasia.

Watu walioko ndani na nje ya nchi hiyo wanahofia kuwa mara Marekani pamoja na washirika wao hawatakuwa na shaka tena na maisha ya wanajeshi wao kufariki nchini Afghanistan baada ya kuondoa majeshi hayo mwaka 2014, nchi hiyo inaweza kuachwa kutumbukia katika mikono ya wababe wa kuuza madawa ya kulenywa na makundi yenye imani kali za kidini.

US Secretary of State Hillary Rodham Clinton waves as she arrives for a meeting of the Action Group for Syria at the European headquarters of the United Nations, UN, in Geneva, Switzerland, Saturday, June 30, 2012. The United States and Russia failed on Friday to bridge differences over a plan to ease Syrian President Bashar Assad out of power, end violence and create a new government, setting the stage for the potential collapse of a key multinational conference that was to have endorsed the proposal. (Foto:Keystone, Laurent Gillieron/AP/dapd)
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Hillary ClintonPicha: AP

Marekani kuendelea kuisaidia Afghanistan

Serikali ya rais Barack Obama italiomba baraza la Congress kuendeleza msaada wa Marekani kwa Afghanistan karibu na kiwango ilichokuwa ikitoa katika muongo mmoja uliopita hadi mwaka 2017 kama sehemu ya juhudi za kimataifa kuimarisha nchi hiyo hata pale ambapo majeshi ya kimataifa yataondolewa katika muda wa miaka miwili ijayo.

Viongozi kutoka mataifa 80 pamoja na mashirika ya kimataifa waliokusanyika mjini Tokyo, mji mkuu wa Japan , wanatarajiwa kuidhinisha kile kinachojulikana kama , azimio la Tokyo, linalopendekeza kuungwa mkono pamoja na kutoa fedha kwa serikali ya mjini Kabul.

Mwandishi : Sekione Kitojo / afpe/ ape

Mhariri : Bruce Amani