1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uturuki na Marekani zajadili kusitisha mapigano Gaza

21 Agosti 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan na mwenzake wa Marekani, Antony Blinken wamejadiliana kuhusu juhudi mpya za kutafuta makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza, kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hamas.

https://p.dw.com/p/4jj88
Mzozo kati ya Israel na Hamas | Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken akutana na rais wa Misri Abdel-Fattah Al-Sissi
Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken, akutana na Rais wa Misri Rais wa Misri Abdel-Fattah el-Sissi huko El-Alamein, Misri, Agosti 20, 2024Picha: Egyptian President Office/APAimages/IMAGO

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Uturuki, Oncu Keceli amesema mazungumzo hayo yaliyofanyika kwa njia ya simu, yametokana na ombi la Marekani. Amesema Fidan na Blinken pia wamejadiliana kuhusu maendeleo ya kikanda. Wakati huo huo, kundi la Hezbollah la nchini Lebanon leo limerusha zaidi ya roketi 50, na kushambulia nyumba kadhaa binafsi katika Milima ya Golan inayokaliwa na Israel. Shambulizi hilo limefanyika siku moja baada ya Blinken kukutana na wapatanishi wa Misri na Qatar, wakati akiendeleza juhudi za kidiplomasia kuhakikisha vita vinasitishwa Gaza. Nalo jeshi la Israel limesema limefanya mashambulizi ya mabomu katika maghala ya kuhifadhia silaha ya Hezbollah kwenye Bonde la Bekaa nchini Lebanon.