1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wachezaji wa zamani watumai kuipa Ujerumani ushindi

7 Julai 2022

Ujerumani imeingia kwenye michuano ya UEFA 2022, huku wachezaji wa zamani wakitumia uzoefu wao kuiwezesha timu hiyo kurudi tena kwenye ushindi.

https://p.dw.com/p/4Dmyg
FIFA Fussball Weltmeisterschaft 2019 der Frauen I Sara Daebritz  und Svenja Huth
Picha: Alex Gottschalk/DeFodi/IMAGO

Sara Däbritz akiwa na umri wa miaka 18, kwa mara ya kwanza aliichezea Ujerumani wiki moja kabla ya kuanza kwa mashindano timu ya mpira wa miguu ya wanawake barani Ulaya mnamo mwaka 2013.

Mwezi mmoja baadaye, alivishwa medali ya ushindi shingoni mwake baada ya taifa hilo kushinda taji lake la sita mfululizo la Ulaya.Kwa sasa Däbritz ana umri wa miaka 27, ni mmoja wa viongozi katika timu ya mpira wa miguu ya wanawake yenye sura mpya.

Anaamini kwamba watarejea kwenye ushindi baada ya kipindi cha mpito.Kushuka kwenye nafasi ya ushindi kwenye timu hiyo mwaka 2017 na 2019 ni chanzo cha mafanikio ya siku zijazo.

Kwanini timu ya wanawake ya Ujerumani imeshuka viwango?

"Tulikuwa na timu mpya, isiyo na uzoefu na tulihitaji muda zaidi wa kujiendeleza," alisema Dabritz alipozungumza na DW.

"Sasa nadhani tumejitayarisha zaidi. Tuna timu yenye uzoefu na pia wachezaji wachanga wenye vipaji." alisema na kuongeza kuwa anataka kuonyesha uwezo wake uwanjani na ndoto yao  ni kushinda ligi ya UEFA.

Pembeni yake atakuwepo Svenja Huth, ambaye hakuwa mchezaji mwaka 2013 wakati timu hiyo iliposhinda.

Kiungo huyo ameshinda mataji matatu kwenye ligi kuu ya Ujerumani ya Bundesliga na mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa. Pia amepata  medali ya dhahabu katika Olimpiki mwaka 2016.

Fußball | Frauen | Deutschland - Schweiz | Sara Daebritz
Picha: Karina Hessland/IMAGO

Kulingana na Svenja Huth alisema "nimeshinda sana, lakini nimepitia vikwazo na shinikizo la mashindano"Alisema na kuongeza kwamba  "Nataka niwahamasishe wachezaji chipukizi ambao hawajawahi kuwa na hali kama hii."

Ujerumani ilitolewa katika robo-fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2019 na ligi ya mabingwa barani Ulaya mwaka 2017. "Mwaka 2017, tulichuana dhidi ya Denmark, tulichukua ubingwa na tulizingatia," Huth alisema.

Däbritz na Huth wanaamini kwamba Ujerumani inachochea morali katika timu yake ili kupata ushindi.

"Umoja  katika timu ni muhimu," Däbritz alisema. "Tumefahamiana zaidi na tuna mazingira mazuri uwanjani.

Huth alisema timu hiyo haihisi shinikizo la kuchukua ushindi kama ilivyokuwa zamani,kwa sababu ushindi huo hauwezekani tena."Soka ya wanawake imeendelea, ubora umeimarika na pengine kuna mataifa saba au manane ambayo yanaweza kushinda taji," Huth alisema.

Wachezaji wote wawili tayari wameandika historia mnamo 2013 na sasa wanatarajia kuiandika tena katika wakati ambapo soka la wanawake linakua kwa kasi.Kurudi katika ushindi katika wakati huu,kunaweza kuwa na athari kubwa kuliko ushindi wa mataji sita mfululizo ya zamani nchini Ujerumani.