1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wabunge wa Uhispania waanza kujadili muswaada wa msamaha

13 Desemba 2023

Wabunge wa Uhispania wameanza kuujadili muswaada tete wa sheria ambao utatowa msamaha kwa raia wa nchi hiyo wanaopigania kujitenga kwa jimbo la Katalunya

https://p.dw.com/p/4a5nk
Waziri Mkuu wa Uhispania, Pedro Sanchez.
Waziri Mkuu wa Uhispania, Pedro Sanchez.Picha: Manu Fernandez/AP Photo/picture alliance

Kutolewa kwa msamaha kwa wanasiasa wa jimbo hilo tajiri ilikuwa sehemu ya ahadi za Waziri Mkuu Pedro Sanchez kusalia madarakani.

Mjadala huo ulioanza jioni ya jana, unafanyika ikiwa ni miaka sita tangu jaribio lililoshindwa la kutangaza uhuru wa Katalunya, huku Sanchez akisema msamaha huo utasaidia kufunguwa ukurasa mpya.

Soma zaidi: Uhispania baada ya Uchaguzi wa Bunge

Wabunge 178 kati ya 350 waliridhia kuanza kujadiliwa kwa msamaha huo. Wabunge hao pia waliridhia kuanzishwa kwa kamisheni tatu zinazotakiwa na vyama vinavyopigania kujitenga kwa Katalunya, ili kuiunga mkono serikali ya mseto ya Sanchez.

Mojawapo ya kamisheni hizo ni ile ya kuchunguza kashfa ya ujasusi dhidi ya viongozi wa Katalunya kupitia programu ya Pegasus baada ya kushindwa kwa jaribio la uhuru mwaka 2017.