1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Chama cha Republican huenda kikatafakari kumuondoa Joe Biden

26 Julai 2023

Spika wa bunge la Marekani Kevin McCarthy amesema huenda wabunge wa chama cha Republican wakatafakari hatua ya uchunguzi kumwondoa madarakani rais Joe Biden kutokana na madai ya utovu wa nidhamu katika masuala ya fedha.

https://p.dw.com/p/4UPPY
US-Präsident Joe Biden
Picha: Antti Aimo-Koivisto/Lehtikuva/dpa/picture alliance

Wabunge wa chama cha Republican wapo chini ya shinikizo kubwa wakitakiwa na chama chao kuonyesha msimamo wa  kumuunga mkono Donald Trump kabla ya uchaguzi wa rais wa mwaka ujao nchini Marekani.

Spika Maccarthy asema madai ya fedha yapaswa kuchunguzwa

Spika Mccarthy amesema bungeni kwamba mambo yanayotajwa na wabunge wa chama cha Republican juu ya masuala ya fedha ya familia ya rais Biden yanapaswa kuchunguzwa.

Bunge halijathibitisha kosa lolote

Hata hivyo Spika McCarthy amekiri kwamba mpaka sasa bunge halijathibitisha kosa lolote lakini amesema uchunguzi unaliwezesha bunge kupata taarifa na hivyo kubainisha ukweli.