1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSenegal

Senegal: Wabunge wapitisha mswada wa kuahirisha uchaguzi

6 Februari 2024

Wabunge nchini Senegal wamepiga kura ya kuunga mkono mswada wa kuahirisha uchaguzi mkuu ambao sasa umepangwa kufanyika Desemba 15 mwaka huu.

https://p.dw.com/p/4c56D
Senegal - Maandamano ya kupinga hatua ya kuahirisha uchaguzi
Maandamano yenye vurugu yameendelea kushuhudiwa Senegal kufuatia uamuzi huo wa kuahirisha uchaguzi: 04.02.2024Picha: Seyllou/AFP

Wabunge kadhaa wa upinzani walizusha vurugu ili kujaribu kukwamisha mchakato huo, lakini hatimaye wabunge 105 kati ya 165 waliunga mkono mswada huo. Hatua hii itamuwezesha rais Macky Sall ambaye anakamilisha mihula yake miwili, kusalia madarakani hadi mrithi wake atakapopatikana.

Hii ni mara ya kwanza kwa taifa hilo kuahirisha uchaguzi, jambo ambalo limezusha hasira na vurugu kutoka upinzani wanaodai kuwa hatua hiyo ni sawa na mapinduzi.

Soma pia: Watu waandamana Senegal kupinga uamuzi wa Rais kuahirisha uchaguzi

Hatua hii imezusha maandamano mapya mjini Dakar na kupelekea hadi baadhi ya shule kufungwa. Awali, uchaguzi wa rais nchini Senegal ulikuwa umepangwa kufanyika tarehe 25 mwezi wa Februari.