1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaCameroon

Yaounde: Waasi wanaotaka kujitenga wameua raia 10

18 Julai 2023

Waasi wanaotaka kujitenga wameua raia 10 na kuwajeruhi wengine wawili katika mmoja ya mikoa tete inayozungumza Kiingereza nchini Cameroon, kulingana na wizara ya ulinzi ya nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4U3VY
Rais wa Cameroon Paul Biya
Rais wa Cameroon Paul BiyaPicha: Jemal Countess/UPI/newscom/picture alliance

Kanali wa wizara hiyo Cyrille Atonnfack, amesema waasi kadhaa waliovalia sare zinazofanana na za jeshi wakiwa na bunduki za kisasa, waliwachukuwa watu nje ya baa katika mji mkuu wa mkoa wa Northwest, Bameda, Jumapili jioni, na kuanza kuwafyatulia risasi, na pia kuwajeruhi wateja kadhaa waliokuwa wamekaa kwenye meza klabuni hapo.

Mamlaka zimefungua uchunguzi juu ya mauaji hayo

Wizara hiyo imesema mamlaka zimefungua uchunguzi juu ya mauaji hayo, na kuongeza kuwa operesheni zinaendelea kuwasaka wauaji. Mikoa ya nchi hiyo inayozungumza Kiingereza ya Northwest na Southwest imekumbwa na mzozo tangu waasi wanaotaka kujitenga kutangaza uhuru mwaka 2017, baada ya miongo kadhaa ya malalamiko kuhusiana na ubaguzi wa serikali inayodhibitiwa na wazungumzaji wa Kifaransa.

Rais Paul Biya amekataa miito ya mikoa hiyo kupatiwa mamlaka zaidi

Rais Paul Biya, ambaye ameitawala nchi hiyo ya Afrika ya Kati kwa mkono wa chuma kwa miaka 40, amekataa miito ya mikoa hiyo kupatiwa mamlaka zaidi, na badala yake kuendesha ukandamizaji zaidi.