1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wa Yemen watishia kuzishambulia meli za Israel

10 Desemba 2023

Waasi wa Houthi nchini Yemen wanaoungwa mkono na Iran, wametishia kushambulia chombo chochote kitakachoelekea katika Bandari za Israel hadi pale chakula na dawa, zitakaporuhusiwa kuingia katika eneo la Gaza.

https://p.dw.com/p/4ZzGK
Yemen Houthi
Wapiganaji wa Houthi Picha: Khaled Abdullah/REUTERS

Katika taarifa yao walioituma katika mitandao ya kijamii waasi hao walisema haijalishi ni bendera gani itakayokuwa inapepea katika meli hizo, au uraia wa wamiliki wa meli hizo au hata wale wanaoendesha operesheni zake, meli zinazoelekea Israel zitalengwa. 

Onyo hilo limekuja wakati kukiwa na wasiwasi kwenye Bahari ya shamu, kufuatia misururu ya mashambulizi yanayofanywa na waasi hao wa Houthi tangu kuanza kwa vita kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas Oktoba 7. 

Meli ya kivita ya Marekani yazuia mashambulizi ya Wahouthi

Waasi hao wamekuwa wakizishambulia meli wanazodhani zina mafungamano ya moja kwa moja na Israel. 

Kundi la Hamas limekaribisha uamuzi wa wahouthi waliouita wa kijasiri.