1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wa M23 wapuuza wito wa Viongozi wa EAC

Benjamin Kasembe 30 Machi 2023

Waasi wa M23 wamepuuza matakwa ya viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kuwashinikiza kuwataka kuondoka kwenye maeneo wanayoyashikilia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo katika kipindi cha mwezi mmoja.

https://p.dw.com/p/4PUi0
DR Congo Kongolesische Jugendliche schließen sich der Armee an, um Rebellen zu bekämpfen
Picha: Benjamin Kasembe/DW

Kama ilivyotakiwa na viongozi hao wa nchi za jumuiya ya afrika mashariki huko mjini Addis ababa mwezi wa februari,waasi  M23 wamekaidi amri hiyo ya kuondoka kwenye maeneo wanayoshikilia na hivi sasa wanaendelea kujiimarisha.

Kundi hilo linaongeza nguvu katika sehemu  tofauti za wilaya za rutshuru na masisi ambako wameendelea kuzishambulia ngome za jeshi tiifu kwa serikali.

Watu 5 wauawa katika shambulizi la majambazi mashariki mwa DRC

Hata hivyo, katika miiji ya Kitshanga hali imezidi kuwa mbaya zaidi kutokana na vurugu zinazo shuhudiwa kila kukicha, na raia wengi wana wasiwasi na maisha yao.

Wakati huohuo, siku ya juma tatu waasi hao waliuteka upya mji mdogo wa mweso kilometa 15 magharibi mwa mji wa kitshanga ambamo mapigano makali yalishuhudiwa kati yao na jeshi la congo nakuongeza kishindo kwa wananchi waliolazimika kukimbilia porini.pamoja nakuitumainia serikali kwa upatikanaji wa Amani.

DRC: Mauaji dhidi ya raia yanaendelea licha ya uwepo wa vikosi vya usalama

Huku hayo yakiendelea ,wanajeshi wa UPDF kutoka nchini uganda watarajiwa pia kuwasili wilayani Rutshuru kupitia mji wa bunagana kwenye mpaka  kati ya congo na nchi hiyo, ambamo watahudumu chini mwavuli wa nchi za jumuiya ya afrika mashariki kwakuleta amani mashariki ya congo.

Hata hivyo, hadi mchana huu  waasi wa M23 wamezishambulia ngome za jeshi la congo kando na mji wa mweso ambamo milio ya risasi ilianza kusikika tangu asubuhi ya leo alhamisi.

Mwandishi: Benjamin Kasembe