1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wa M23 wakabiliana na jeshi la Kongo

23 Februari 2023

Waasi wa M23 wamesonga mbele katika mapigano yao dhidi ya jeshi la Kongo na kuukaribia mji wa Mushaki ulioko umbali wa kilometa 15 kaskazini mwa mji wa Sake wilayani Masisi

https://p.dw.com/p/4Ns3Q
Demokratische Republik Kongo | Soldaten in Maisi
Picha: Alain Uaykani/Xinhuaa/picture alliance

Hadi jana jioni jeshi la Kongo lilitumia ndege za kivita kuzishambulia ngome za kundi hilo kando na mji huo wa Mushaki na kupelekea maelfu wa raia kukimbia makaazi yao wakielekea tena Goma.

Mapigano baina ya jeshi la DRC na waasi wa M23 yazuka licha ya miito ya kusitisha vita

Mapigano hayo yalianza  tangu asubuhi ya jana juma tano, ambapo waasi wa M23 walishambulia kambi ya jeshi la Kongo iliyoko  kwenye mlima wa Mushununu takribani kilometa 15 Kutoka mushaki kwenye barabara  ya Goma kuelekea Masisi ya kati.

Hadi mchana kati wa jana, maelu wa raia waliokuwa wakiuacha mji wa Mushaki walielekea Sake na wengine kadhaa kuwasili masaa za jioni katika mji wa Goma 

DR Kongo | Kenianische Truppen in Goma
Vikosi vya Kenya ni sehemu ya jeshi la kikanda KondoPicha: Jane Barlow/PA Wire/empics/dpa/picture alliance

Ikiwa baadhi ya wananchi wamejihifadhi kwenye familia za mapokezi na hata kujenga mahema kando na barabara ,wengine wameendelea kuhangaika ndani ya kambi ya wakimbizi inje kidogo na mji wa Goma lakini bila huduma yoyote ya chakula na maji safi . elezea mama huyu iliye wasili hapa baada ya masaa kadhaa akitembea kwa mguu.

Hata hivyo, jeshi tiifu kwa serikali  lililazimika kuanza kutumia  helikopta zilizo vurumisha  mizinga kuelekea  vijiji vya kausa na Ruvunda ambavyo waasi hao walikuwa wamedhibiti. kulingana na mashirika yakiraia, waasi wa M23 wanaongeza sasa  nguvu kwa lengo lakuliteka eneo kubwa la migodi Rubaya moja kati ya machimbo makubwa ya mdini nchini congo upande wa wabunge mkoani kivu kaskazini ,wameendela kukituhumu kikosi cha kikanda kwa kufumbia macho vita hivyo vinavyo endelea kusambaa kama anavyo sema MUHOZI NGARUYE mchaguliwa wilayani Rusthuru.

Ikiwa waasi watafanikiwa kuidhibiti barabara inayoelekea Mushaki huenda kukatatize pakubwa shughuli zote za usafiri nakuuweka mji huu wa Goma unao kadiria zaidi ya watu milioni moja katika shida la njaa.

Benjamin Kasembe, DW Goma