1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wa M23 wachukua udhibiti wa mji ulio karibu na Goma

25 Novemba 2023

Kundi la waasi la M23 limeuteka hapo jana mji wa kimkakati wa Mweso karibu na mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://p.dw.com/p/4ZRE8
DR Kongo Soldaten
Wanajeshi wa DRC huko Kibumba:30.11.2022Picha: Alain Uaykani/Xinhua/IMAGO

Hayo ni kulingana na taarifa iliyotolewa na wakazi wa mji huo ulio karibu kilometa 60 kaskazini mwa Goma.

Jeshi la Kongo FARDC pamoja na wanamgambo washirika limekuwa likipambana na M23 mashariki mwa nchi hiyo na hivyo kuwaweka katika mazingira hatarishi wakazi na wakambizi wa ndani  huko Goma.

Umoja wa Mataifa na baadhi ya nchi za Magharibi wanasema Rwanda inawaunga mkono M23, madai ambayo yamekuwa mara kadhaa yakikanushwa na serikali ya Kigali. Wagombea wa uchaguzi wa urais unaotarajiwa Desemba 20 huko Kongo, wameanza ziara zao za kampeni mashariki mwa nchi hiyo licha ya mapigano kuripotiwa sehemu mbalimbali.