1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroYemen

Waasi wa Houthi wasema wataanza kuzilenga meli za Marekani

16 Januari 2024

Kundi la waasi wa Houthi wa nchini Yemen limesema linatanua operesheni zake kwenye Bahari ya Shamu ikiwa ni pamoja na kuzilenga meli za mizigo za Marekani zinazotumia ujia huo muhimu wa maji duniani.

https://p.dw.com/p/4bHmk
Meli ya mizigo ikikatisha Bahari ya Shamu
Waasi wa Houthi wamekuwa wakizilenga meli za mizigo kwenye njia ya Bahari ya Shamu.Picha: Houthi Media Centre/AFP

Hayo yamesemwa na msemaji wa waasi wa Houthi, Nasruldeen Amer, saa chache baada ya kundi hilo kuishambulia meli ya mizigo ya Marekani kwa kombora la masafa.

Amesema meli za Marekani pamoja na Uingereza zitakuwa sehemu ya hujuma za kundi hilo kutokana na mashambulizi yaliyofanywa na mataifa hayo mawili dhidi ya ngome za waasi wa Houthi nchini Yemen.

Hapo kabla kundi hilo lilidai kwamba linazilenga pekee meli za mizigo zinazoelekea Israel pamoja na bandari za Ukingo wa Magharibi kwa malengo ya kuishinikiza Israel isitishe operesheni yake ya kijeshi huko Ukanda wa Gaza.

Marekani na Uingereza zilijibu hujuma hizo za Wahouthi kwa kufanya mashambulizi ndani ya Yemen mnamo juma lililopita.