1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waarmenia waandamana kumtaka waziri mkuu ajiuzulu

27 Mei 2024

Makumi kwa maelfu ya waandamanaji walikusanyika jana katikati ya mji mkuu wa Armenia, Yerevan, wakimtaka Waziri Mkuu Nikol Pashinyan ajiuzulu.

https://p.dw.com/p/4gJF6
Maandamano ya Waarmenia mjini Yerevan
Maelfu ya Waarmenia wamekuwa wakiandanama wakimtaka Waziri Mkuu Nikol Pashinyan ajiuzuluPicha: Alexander Patrin/ITAR-TASS/IMAGO

Hii ni baada ya Armenia kukubali kuikabidhi Azerbaijanudhibiti wa vijiji kadhaa vya mpakani. Maandamano hayo yalikuwa ya karibuni katika wiki ya msururu wa mikusanyiko iliyoongozwa na mhubiri mashuhuri katika Kanisa la Mitume la Kiarmenia, Bagrat Galstanyan, askofu mkuu wa jimbo la Tavush, kaskazini mashariki mwa Armenia.

Aliongoza kuundwa kwa vuguvugu linalojulikana kama Tavush For The Homeland vaada ya Armenia mnamo Aprili kukubali kuwachia udhibiti wa vijiji vinne katika eneo la Azerbaijan. Ijapokuwa vijiji hivyo vilikuwa suala kuu la kuundwa vuguvugu hilo, limetanuka na kuelezea malalamiko mengine kuhusu Pashinyan na serikali yake.

Viongozi wa vuguvugu hilo wameuambia mkutano wa jana kuwa wanaunga mkono Galstanyan kuwa waziri mkuu mpya. Uamuzi wa kuvikabidhi vijiji hivyo vya Tavush ulifuatia operesheni kali ya kijeshi Septembamwaka jana ambapo jeshi la Azerbaijan liliwalazimu maafisa wa Kiarmenia wanaopigania kujitenga katika mkoa wa Karabakh kusalimu amri.