1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waangola wapiga kura

1 Septemba 2012

Waangola wamepiga kura Ijumaa (31.08.2012) katika uchaguzi wa tatu nchini humo tangu uhuru,ambapo rais Jose Eduardo dosSantos akitarajiwa kushinda, licha ya upande wa upinzani kuanza kupata nguvu.

https://p.dw.com/p/161rD
Bürger aus Luanda am Morgen des 31.08 stehen in Luanda an, um ihre Stimme abzugeben. Angola hält die 3. Wahlen in einem Mehrparteiensystem ab seit der Unabhängigkeit 1975. Der erste Kandidat der Liste von der Partei, die am meisten gewählt wird, wird automatisch zum neuen Präsidenten Angolas. Copyright: DW/António Cascais 31.08.2012
Mlolongo wa watu wakisubiri kupiga kura mjini Luanda katika uchaguzi wa Angola 2012Picha: DW

Vingi kati ya vituo 10,000 vya kupigia kura vilivyowekwa katika maeneo ya shule nchi nzima, vilifungwa katika muda muda uliopangwa na zoezi la kuhesabu kura lilianza mara moja.Maafisa wa tume ya uchaguzi wamesema kuwa baadhi ya vituo vya kupigia kura vilibaki wazi kwa muda , bila ya kutoa maelezo zaidi.

Uchaguzi huo umekumbwa na matatizo machache hapa na pale, lakini ni uchaguzi ambao umefanyika kwa mafanikio makubwa ikilinganishwa na uchaguzi uliofanyika mwaka 2008 wakati uchaguzi huo ulihitaji kurefushwa hadi siku ya pili kutokana na mtafaruku katika vituo vya kupigia kura.

Ein Mann gibt seine Stimme am Morgen des 31.08.2012 in Luanda ab. Der angolanische Präsident José Eduardo dos Santos bestreitet eine weitere Amtszeit von 5 Jahren. Er ist schon seit 32 Jahren an der Macht. Bei den letzten Parlamentswahlen 2008 bekam er mehr als 80% der Stimmen. Copyright: DW/António Cascais 31.08.2012
Mpiga kura akiweka kura yake katika sanduku mjini Luanda Angola 2012Picha: DW

Uchaguzi ulienda vizuri

Pedro Verona Pires , mkuu wa kundi la wachunguzi wa uchaguzi kutoka umoja wa Afrika, ameueleza utayarishaji wa uchaguzi huo kuwa wa kuridhisha, akiongeza kuwa hali ya upigaji kura ilikuwa nzuri.

"Kila mmoja anakubali kuwa uchaguzi wa mwaka huu ulikuwa umetayarishwa vizuri zaidi kuliko mwaka 2008," Pires , ambaye pia ni rais wa zamani wa Cape Verde ameliambia shirika la habari la AFP.

UNITA kimeonyesha wasi wasi

Chama cha upinzani cha UNITA kimeeleza wasi wasi wake kuwa waungaji wake mkono wasingekubaliwa kupiga kura kutokana na matatizo katika daftari la wapiga kura, wakati baadhi ya wachunguzi wao wa uchaguzi hawakuruhusiwa kuingia katika vituo vya kupigia kura.

Wapiga kura walikuwa wanawachagua wabunge katika bunge lenye wajumbe 220 nchini humo. Kiongozi wa chama ambacho kitapata kura nyingi moja kwa moja anakuwa kiongozi wa nchi. Hakuna shaka kwamba Dos Santos atafanikiwa kurejea madarakani na kuendelea na uongozi wa nchi hiyo alioshikilia kwa muda wa miaka 33 sasa.

Angola's President Jose Eduardo dos Santos (L) casts his vote as his wife Ana Paula looks on during national elections in the capital Luanda, August 31, 2012. Angolans voted on Friday in a one-sided election expected to keep Eduardo dos Santos at the helm of Africa's No. 2 oil producer, but the long-serving leader faces swelling popular pressure to share the nation's riches more evenly. REUTERS/Siphiwe Sibeko (ANGOLA - Tags: POLITICS ELECTIONS)
Rais Jose Eduardo dos Santos akipiga kuraPicha: Reuters

Chama chake cha People's Movement for the Liberation of Angola, MPLA kilipata zaidi ya asilimia 80 ya kura katika uchaguzi wa mwaka 2008, uchaguzi ambao ulionekana kuwa ni halali na baadhi ya wachunguzi licha ya matatizo kadha katika vituo vya uchaguzi. Dos Santos ametumia miongo kadha akiwa kiongozi wa nchi hiyo kuweka madaraka mikononi mwake. Familia yake hususan mwanawe wa kike Isabel, ametumia utajiri mkubwa wa mafuta nchini Angola kujenga himaya ya kibiashara ya kimataifa.

Ujenzi mpya

Pia amemimina mabilioni ya dola katika kuijenga upya Angola baada ya miaka 41 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, ikiwa ni pamoja na miaka 14 ya mapambano ya ukombozi dhidi ya utawala wa kikoloni wa Ureno na hatimaye kuingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa muda wa miaka 27 baada ya uhuru mwaka 1975. Ametumia udhibiti wake katika vyombo vya habari vya taifa kuonyesha mabarabara , mabwawa ya kufua umeme, mashulre na zahanati vilivyojengwa tangu mapigano yalipomalizika muongo mmoja uliopita.

Isaias Samakuva, leader of Angola's main opposition UNITA party , addresses supporters during the party's last rally ahead of parliamentary elections in Viana, about 30 km (19 miles) east of the capital Luanda, August 29, 2012. Angolans will go to the polls on Friday to elect lawmakers and their president. REUTERS/Siphiwe Sibeko (ANGOLA - Tags: POLITICS ELECTIONS)
Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha UNITA Isaiaas SamakuvaPicha: Reuters

Maisha nchini Angola kwa kiasi kikubwa yamekuwa bora. Uchumi katika muda wa muongo mmoja uliopita umekuwa miongoni mwa uchumi unaokuwa kwa kasi kabisa duniani. Pato jumla la taifa kwa mwaka limefikia karibu dola bilioni 1.9 katika mwaka 2009, na kuchupa mara tatu kutoka ukuaji mwaka 2000. Matarajio ya maisha ya watu yamepanda kutoka kiasi cha miaka 40 mwaka 1980 na kufikia kiasi cha miaka 51 hivi sasa.

Matokeo ya awali yanatarajiwa kutolewa Jumamosi mchana (01.09.2012), amesema mkuu wa tume ya taifa ya uchaguzi. Matokeo kamili yanatarajiwa kutolewa wiki ijayo.

Mwandishi : Sekione Kitojo / afpe

Mhariri: Idd Ismail Ssessanga