1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waandamanaji wavamia jengo la bunge Kenya

25 Juni 2024

Mamia kadhaa ya waandamanaji mjini Nairobi wamvunja vizuizi vya usalama na kuvamia majengo ya bunge wakati wa maandamano ya kupinga sheria mpya ya kodi.

https://p.dw.com/p/4hVF6
Kenia | Nairobi
Waandamanaji wavamia majengo ya bunge nchini Kenya Picha: LUIS TATO/AFP/Getty Images

Magari kadhaa ya polisi na sehemu ya jengo la bunge vilichomwa moto katika tukio ambalo limeripotiwa sambamba ripoti za mashambulizi ya risasi ambamo watu wanaripotiwa kuuawa na wengi kujeruhiwa. Huyu hapa ni mmoja wa waandamanaji ambae hakutajwa jina.

"Serikali inatuchukulia kama wageni mahali hapa, tunaukataa muswada huo, kila kifungu, hatuombi marekebisho yoyote, tunaomba waukatae. tutayatwaa mamlaka kwa mikono yetu wenyewe, wala hatuogopi."

Waandamanaji kadhaa wauwawa Kenya

Kwa mujibu wa Tume ya Haki za Kibinadamu ya Kenya, muandamanaji mmoja ameuwawa kwa risasi na wengine watatu kujeruhiwa vibaya.