1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waandamanaji wataka kuondolewa vizuizi Ngorongoro

Veronica Natalis
9 Agosti 2023

Shughuli za kiuchumi zimezorota kufuatia maandamano ya wakaazi huko wilayani Ngorongoro mkoni Arusha, kufuatia kile kinachodaiwa ni maagizo ya serikali yaliotajwa kuwa yanaweka vizuizi vya maendeleo kwa wakaazi.

https://p.dw.com/p/4UxH2
Afrika Tansania Protest Maasai
Picha: DW

Zaidi ya wakazi 1000 wa wilaya na Ngorongoro mkoani Arusha wamekuwa wakiandamana kwa siku tatu mfululizo sasa wakiishinikiza serikali kuondoavikwazo vilivyowekwa katika baadhi ya maeneo, vikwazo vinavyozuia ujenzi na uendelezaji wa shughili za maendeleo kama vile shule, hospitali, barabara, maji na makazi binafsi.

Inadaiwa tangu mwaka 2021 serikali ya Tanzania ilisitisha shughuli hizo kwa sababu ambazo hazijawekwa wazilakini wakazi wenyewe wa Ngorongoro wanasema wamesitishiwa huduma ili kuyahama makazi yao.

Soma pia:Serikali ya Tanzania imesema hakuna mapambano yoyote kati ya askari polisi na wananchi

Wananchi wa eneo la Endulen wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha Tanzania kwa siku ya tatu sasa wanajaribu kutuma ujumbe kwa serikali ya Tanzania ya kuondoa zuio ambalo wanasema linawanyima haki za msingi za kimaendeleo.

Hoja ya kutoendelezwa kwa maeneo

Inadaiwa kwamba tangu mwaka 2021, kumekuwa na maagizo ya serikali kutoka ngazi tofauti yakizuia ujenzi na uendelezaji wa majengo binafsina huduma za kijamii hali ambayo inaleta athari katika Maisha ya jamii hiyo ya wafugaji ya maasai.

Barua iliyoandikwa na ofisi ya halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro na kusainiwa na mkurugenzi wa wilaya hiyo Dr. Juma Mhina mwaka 2021, ilielekezwa kwa shule tatu za sekondari wilayani humo  zikiwemo  Nainokanoka na shule ya sekondari ya wasichana Ngorongoro, ilitoa agizo la kuhamishwa kwa fedha za miradiya Uviko 19 na kwenda halmashauri ya wilaya ya Handeni mkoani Tanga.

Soma pia:Tanzania yatuhumiwa kuzuia huduma za jamii Ngorongoro

Hali hiyo inatajwa na wanasheria kuwa ni mwendelezo ya kunyima haki kwa jamii hiyo ya Maasai. 

Hakuna mwitiko wa serikali wa moja kwa kuhusu maandamano hayo, lakini mara kadhaa serikali ya Tanzania imekuwa ikikanusha madai ya kuwatesa na kuwanyima haki za msingi wakazi hao.