1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPeru

Waandamanaji Peru wamg'ang'ania rais aondoke

25 Januari 2023

Maelfu ya waandamanaji wameingia mitaani katika mji mkuu wa Peru Lima na kukabiliana na polisi, saa chache baada ya rais Dina Boluarte kutoa wito wa mapatano baada ya miezi miwili ya maandamano.

https://p.dw.com/p/4Mh5N
Politische Krise in Peru
Picha: Klebher Vasquez/AA/picture alliance

Maelfu ya waandamanaji waliomiminika barabarani mjini Lima, wamekabiliwa na maafisa wa polisi kwa kurushiwa gesi ya kutoa machozi saa chache baada ya rais wa  Peru, Dina Boluarte  kutoa wito wa kitaifa wa usitishwaji uhasama baada ya takriban miezi miwili ya maandamano.

Maandamano ya kuipinga serikali yaliyofanyika jana nchini humo ndio yaliokuwa makubwa na yaliojaa ghasia tangu yale ya siku ya Alhamisi wiki iliyopita, wakati makundi makubwa ya watu wengi kutoka maeneo ya Andean walipomiminika mjini Lima wakitaka rais Boluarte  kujiuzulu, kufanyika kwa uchaguzi wa haraka na kuvunjwa kwa bunge.

Waandamanaji wamekasirishwa na kuuwawa kwa zaidi ya wenzao 40 kufuatia machafuko yaliyozuka tangu rais wa zamani Pedro Castillo kuondolewa madarakani kwa nguvu mwezi uliopita kwa madai ya kuhusika na uasi alipojaribu kulivunja bunge.