1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waafrika Kusini wanapiga kura katika uchaguzi mkuu wa bunge

29 Mei 2024

Waafrika Kusini wanapiga kura katika zoezi la uchaguzi mkuu wa bunge lililoanza leo.Rais Cyril Ramaphosa baada ya kuwasili katika kituo chake cha kupigia kura asubuhi alisema zoezi hilo linakwenda vizuri.

https://p.dw.com/p/4gPlu
Cyril Ramaphosa
Rais Cyril Ramaphosa baada ya kuwasili katika kituo chake cha kupigia kura asubuhi alisema zoezi hilo linakwenda vizuri. Picha: Oupa Nkosi/REUTERS

Ni siku nzuri,juwa linawaka na nimesikia kwamba uchaguzi umeshaanza nchi nzima na unakwenda vizuri.Nina furaha kubwa kuwa hapa na mke wangu kuja kupiga kura katika eneo nilikozaliwa kwa idhini ya tume ya uchaguzi.''

Zaidi ya watu milioni 27 wameandikishwa kupiga kura katika uchaguzi huo.
Uchaguzi huo kwa kiasi kikubwa unatarajiwa kuwa tukio la kihistoria kwa nchi hiyo tangu ilipoingia kwenye mfumo wa kidemokrasia, baada ya kumalizika utawala wa ubaguzi wa rangi, kutokana na kura za maoni za hivi karibuni kuonesha chama tawala cha National African congress,ANC kinaungwa mkono kwa sasa na chini ya asilimia 50 ya Waafrika Kusini.

Waafrika Kusini wapiga kura kulichagua bunge jipya

Matokeo hayo yanaashiria huenda chama hicho kikashindwa kwenye uchaguzi huo mkuu kupata wingi mkubwa bungeni kwa mara ya kwanza tangu kilipoingia madarakani mwaka 1994.
 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW