1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Vurugu zazuka baada ya polisi wa Israel kuingia msikitini

5 Aprili 2023

Polisi ya Israel imewakamata zaidi ya watu 350 baada ya vurugu kuzuka katika eneo tete la msikiti wa Al-Aqsa,mjini Jerusalem mapema leo.

https://p.dw.com/p/4PiVO
Israel | Viunga vya Msikiti wa Al-Aqsa mjini Jerusalem
Polisi wa Israel wakimuondoa mwanaume wa Kipalestina kutoka viunga vya msikiti wa Al-Aqsa mjini Jerusalem.Picha: AHMAD GHARABLI/AFP/Getty Images

Maafisa waliingia katika msikiti huo na  kuwaondoa watu iliowaita wachochezi. Polisi ya Israel imesema walilazimika kuingia kwenye msikiti huo baada ya vijana waliokuwa wanavunja sheria na wachochezi waliokuwa wamefunika nyuso, kujifungia ndani.

Taarifa ya polisi imesema vijana hao walitaka kuvuruga utulivu wa umma na kuuchafua msikiti.

Wanamgambo wa kipalestina walijibu kwa kufyatua makombora kuelekea Israel kutokea Ukanda wa Gaza unaodhibitiwa na Hamas, hatua iliyochochea mashabulizi ya kutokea angani ya Israel.

Vurugu hizo zimejiri wakati hofu ikiwa imetanda katika eneo la Jerusalem Mashariki huku mwezi Mtukufu wa Ramadhan ukienda sanjari na Siku Kuu ya Pasaka ya Kiyahudi.

Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imelaani uvamizi huo wa vikosi vya Israel katika msikiti wa Al Aqsa ikisema mbinu za aina hiyo zitachochea makabiliano zaidi na Wapalestina.