1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Von der Leyen: Umoja wa Ulaya utasimama na Ukraine

8 Julai 2023

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen ameadhimisha siku 500 za uvamizi wa Urusi nchini Ukraine kwa ahadi ya kuendelea kusisimama pamoja na serikali mjini Kyiv bila kikomo.

https://p.dw.com/p/4Tcew
EU-Haushalt
Picha: Virginia Mayo/dpa/picture alliance

Kupitia ujumbe kwa njia ya mtandao wa Twitter aloutuma hii leo ambayo ni siku ya 500 tangu Urusi ilipotuma vikosi vyake ndani ya ardhi ya Ukraine.Von der Leyen amesema kipindi hicho kimeakisi utayari wa Ukraine kujilinda na mshikamano usioyumba kutoka Umoja wa Ulaya.

Soma zaidi:Umoja wa Ulaya kuisaidia Ukraine kujiunga na Umoja huo

Wakati huo huo  rais Volodymyr Zelensky ametumia siku ya leo kuisifu nchi yake kwa kusimama imara dhidi ya uvamizi wa Urusi na kuapa kuwa nchi hiyo kamwe "haitadhibitiwa na wavamizi". Zelensky ametoa ujumbe huo alipokitembelea kisiwa kidogo cha Bahari Nyeusi kinachotajwa kuwa alama ya upinzani wa Ukraine dhidi ya uvamizi wa Urusi.