1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiItaly

Von der Leyen na Meloni kukitembelea kisiwa cha Lampedusa

16 Septemba 2023

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen anapanga kwenda Italia baadaye leo baada ya taarifa za kuwasili kwa maelfu ya wahamiaji katika kisiwa cha Lampedusa wiki hii.

https://p.dw.com/p/4WQLX
Italia | Wahamiaji kisiwani Lampedusa
Mamia ya wahamiaji wengi kutoka Afrika hutumia boti za mpira kuvuka bahari ili kuingia barani Ulaya Picha: Cecilia Fabiano/AP Photo/picture alliance

Kwa mujibu wa msemaji wake, von der Leyen atakutana na Waziri Mkuu Giorgia Meloni mjini Roma ambapo wawili hao wanapanga kwa pamoja kukitembelea kisiwa cha Lampedusa .

Jana Ijumaa, Meloni alimwalika Rais huyo wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya ili kushuhudia ukubwa wa tatizo linaloikabili Italia.

Bibi Meloni, kiongozi anayeegemea siasa kali za mrengo wa kulia alitoa wito kwa Ulaya kufanya operesheni haraka ili kukomesha safari za wahamiaji wanaotumia boti kupitia bahari ya Mediterrania. Ametaka wahamiaji hao wasiruhusiwe kuanza safari hizo kutokea Afrika.