1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VITUO VYA SILAHA VYATEMBELEWA

29 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFo8

TRIPOLI: Wakaguzi wa silaha za kinyuklia wa Umoja wa Mataifa wamevitembelea vituo vinavyohusika na mradi wa silaha za kiatomiki za Libya wakijatayarisha kwa ukaguzi kamili katika nchi hiyo ya Afrika ya Kaskazini.Wakaguzi wa Shirika la Kimataifa la Nishati za Kinyuklia-IAEA wakiongozwa na mkuu wa shirika hilo bwana Mohamed El-Baradei waliwasili Tripoli siku ya jumamosi,ikiwa ni wiki moja tu baada ya Libya kukiri kuwa ilijaribu kutengeneza silaha zilizopigwa marufuku,ikiwa ni pamoja na silaha za atomiki.