1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vituo vya kuwahifadhi wahamiaji si jibu sahihi kwa EU

Sekione Kitojo
4 Julai 2018

Vituo vipya vinavyopangwa kujengwa karibu na bahari ya Mediterania kuwahifadhi wahamiaji havitakuwa suluhisho sahihi kwa changamoto za wakimbizi katika mataifa ya Umoja wa Ulaya.

https://p.dw.com/p/30q4n
Rettung von Flüchtlingen - Flüchtlingsschiff "Aquarius
Picha: picture-alliance/dpa/MSF/SOS Mediterranee/K. Karpov

Hayo yamesemwa  na  shirika la uhamiaji la  Umoja  wa  mataifa kuhusiana  na  wazo ambalo shirika  hilo limeombwa  kulitekeleza. 

Wahamiaji  kuvuka bahari  na  kuingia  katika  mataifa  ya  Ulaya wamepungua kwa  kiasi  kikubwa, na  ni  kiasi  ya  watu 45,000 tu ambao  wamefanikiwa  kuingia  Ulaya  mwaka  huu. Lakini  suala hilo  nyeti  kabisa  linapeleka  mbio  ajenda ya  kisiasa  ya  Umoja wa  Ulaya.

Spanien «Aquarius»-Migranten in Valencia
Wakimbizi wakipatiwa huduma ya matibabu baada ya kushuka kutoka katika meli ya Italia ya walinzi wa pwani.Picha: Getty Images/AFP/A. Saiz

Wiki  iliyopita, mataifa  ya  Umoja  wa  Ulaya  yalikubaliana  kubana mipaka  yao  ya  nje  na  kutumia  fedha  zaidi  katika  mataifa  ya Mashariki  ya  kati  na  Afrika  kaskazini kupunguza idadi  ya wanaowasili  katika  mipaka  yao.

Kansela Angela  Merkel , akijaribu  kuokoa muungano  wake unaounda  serikali , siku  ya  Jumatatu  alikubali kuunda  makambi ya  wahamiaji  katika  mipaka  ya  Ujerumani, ikionesha  jinsi  gani Umoja  wa  Ulaya  unashindwa  kukubaliana  kuhusu  sera  ya pamoja  ya  uhamiaji na  serikali  mbali  mbali  zikizidi  kuchukua hatua  za  binafsi.

Kitu  kimoja  viongozi  wa  Umoja  wa  Ulaya  wamekubaliana  ni kuangalia jinsi  ya kujenga  vituo  vya  kufikia ili  kuwahifadhi  wale waliookolewa  kutoka  katika safari  yenye  hatari  ya  kuvuka  bahari ya  Mediterania. Wengi  wanafika  ufukweni nchini  Italia, lakini  zaidi ya  watu 1,300 wamefariki  mwaka  huu.

Türkei Flüchtlingslager in der Stadt Kilis
Kambi ya kuwashikilia wahamiaji nchini UturukiPicha: picture-alliance/dpa/MOKU/U. Onder Simsek

"Bahari  ya  Mediterania ni  eneo linalohusika na  nchi  nyingi, kaskazini  hadi  kusini. Tuna jukumu  la  pamoja  kuongoza kile kinachotokea  katika  eneo  hilo, ikiwa  ni  pamoja  na  kuepuka watu kufa  maji," Euginio Ambrosi , mkuu wa  shirika  la  kimataifa  kwa ajili  ya  wahamiaji, IOM , ujumbe  wa  Umoja  wa  Ulaya aliliambia shirika  la  habari  la  Reuters.

Vipo vituo 10 vya kuwahifadhi wahamiaji

Shirika  la  IOM  pamoja  na  lile  la  Umoja  wa  mataifa  la kuwahudumia  wakimbizi UNHCR, yanatakiwa  kusaidia  katika kuendesha  vituo  hivyo.

Ambrosi  amesema  vituo  10  vilivyopo hivi  sasa  vya kuwahudumia  wahamiaji  nchini  Ugiriki  na  Italia  vinawezekana kuimarishwa  na  vingine  vipya  vinaweza  kuongezwa nchini  Malta. Lakini  kufungua  vipya  katika  eneo  hilo  la  kusini  la  bahari  ya Mediterania , kama  baadhi  ya  mataifa  ya  Umoja  wa  ulaya yanavyotaka, vitachukua  muda.

Libyen Europa Migration Zustände in Flüchtlingslagern
Kituo kimojawapo cha kuwashikilia wahamiaji katika kijiji cha Karareem nchini LibyaPicha: picture-alliance/AP Photo/M. Brabo

Wizara  ya  mambo  ya  ndani  ya  Ujerumani  tayari  inafanyakazi kutayarisha  makubaliano  pamoja  na  mataifa  mengine  ya  Umoja wa  Ulaya  kuwarejesha  wakimbizi nchini ambazo  walijiandikisha kwanza , kuomba  hifadhi, msemaji  wa  wizara  hiyo  amesema leo.

Waziri  wa  mambo  ya  ndani  wa  Ujerumani  Horst Seehofer anatarajiwa  kwenda  Vienna leo, ambako atakutana  na  kansela  wa Austria Sebastian kurz, pamoja  na  waziri  mkuu  wa  Hungary Viktor Orban anatarajiwa  kukutana  na kansela  wa  Ujerumani Angela Merkel  mjini  Berlin.

Wakati  huo  huo, makundi  ya  kutoa misaada  yamesema  mfumo wa  Ufaransa  wa  kuwahudumia  idadi  kubwa  ya  watoto  wahamiaji ambao  hawana  wazazi  hauna mpango maalum na  unawadhuru wale  ambao  wanahitaji  msaada. Ripoti  iliyotolewa  leo , na  shirika la  haki  za  binadamu  la  Human Rights Watch lilieleza  mfumo  huo wenye mkanganyiko  kwamba  unakandamiza watoto.

Belgien - EU-Gipfel in Brüssel - Merkel
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel katika mkutano wa Umoja wa UlayaPicha: picture-alliance/dpa/M. Erd

Kundi la  kutoa misaada  la  madaktari  wasio  na mipaka walisisitiza taarifa  hiyo kwa  kusema kushindwa  kwa  Ufaransa ni  kutokana  na  kufikiria kwamba  mtu  anayedai kwamba  yuko  chini  ya  miaka  18 anadanganya. Watu kiasi  ya  25,000  vijana  wanaodai  hawana watu  waliofuatana  nao  ambao  ni  watoto wahamiaji  waliwasili nchini  humo mwaka  jana.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre / ape

Mhariri: Idd Ssessanga