1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Vita vya Ukraine vyaugubika mkutano wa mawaziri wa G20

1 Machi 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amewasili New Delhi leo pamoja na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov kwa ajili ya mkutano wa nchi 20 zilizostawi na zinazoinukia kiviwanda G20.

https://p.dw.com/p/4O7h3
Josep Borrell
Picha: DW

Mzozo wa Ukraine na mivutano ya Marekani na China inatarajiwa kuzifunika juhudi za mwenyeji wa mkutano huo India kuleta umoja miongoni mwa nchi hizo zenye uchumi mkubwa duniani na zile zinazoinukia.

Blinken amesema hana mpango wowote wa kukutana ana kwa ana na Lavrov katika mkutano huo, ila hii itakuwa mara ya kwanza mawaziri hao wawili kushiriki katika mkutano mmoja tangu mkutano wa G20 huko Bali mwaka jana mwezi Julai.

Lavrov aliwasili India hapo jana jioni na kulingana na wizara ya mambo ya nje ya Urusi, atatumia mkutano huo kuzishambulia nchi za Magharibi.