1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vita vya kuwania ufalme wa Wazulu vyafika mahakamani

Josephat Charo
17 Oktoba 2023

Vita vya kuwania ufalme wa Zulu nchini Afrika Kusini vimefika mahakamani huku kundi moja la familia ya kifalme likijaribu kumuondoa mfalme ambaye hajakamilisha hata mwaka mmoja madarakani.

https://p.dw.com/p/4XeJG
Südafrikan Mangosuthu Buthelezi
Aliyekuwa mfalme wa Wazulu, Mangosuthu Buthelezi.Picha: Rajesh Jantilal/AFP/Getty Images

Mahakama kuu ya Gauteng Kaskazini katika mji mkuu Pretoria inasikiliza hoja za kisheria wiki hii katika vita vya urithi wa kifalme kati ya Mfalme Misuzulu kaZwelithini na binamu yake, mwanamfalme Simakade Zulu, ambaye anaamini ana haki ya kuwa mfamle.

Soma zaidi: Afrika Kusini yajiandaa kwa mazishi ya Mwanamfalme wa Wazulu

Mwanamfalme Simakande anaitaka mahakama ibatilishe hatua ya Rais Cyril Ramaphosa kumtambua Mfalme Misuzulu kama mrithi halali wa kitu cha ufalme, akipinga michakato ya kitamaduni na kisheria iliyofuatwa kumteua Misuzulu.

Mawakili wake wameifahamisha mahakama kwamba uamuzi wa Ramaphosa kumtambua Misuzulu na kumpa cheti kinachostahiki uliharakishwa.

Kesi inatarajiwa kuendelea kusikilizwa kesho Jumatano.