1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Viongozi wakuu duniani waunga mkono uhuru wa Ukraine

17 Juni 2024

Viongozi wa dunia wameunga mkono uhuru wa Ukraine na umuhimu wa kufanyika mazungumzo na Urusi kwa lengo la kuvimaliza vita ingawa wameacha maswali bila majibu ya lini na jinsi mazungumzo hayo yatakavyofanyika.

https://p.dw.com/p/4h75I
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy akilihutubia bunge la Ujerumani, Bundestag mjini Berlin
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy akilihutubia bunge la Ujerumani, Bundestag mjini BerlinPicha: Axel Schmidt/REUTERS

Zaidi ya miaka miwili baada ya Urusi kuivamia Ukraine, viongozi wakuu kutoka zaidi ya nchi 90 duniani, walikutana mwishoni mwa wiki katika eneo la mapumziko la Bürgenstock kwa mkutano wa siku mbili kwa ajili ya kutafuta suluhu ya mzozo mkubwa zaidi barani Ulaya tangu vita vikuu vya pili duniani.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amepongeza mafanikio ya kidiplomasia ya mkutano huo ambao Urusi haikualikwa.

Soma pia: Mkutano wa kimataifa wa amani Ukraine wafungua Uswisi

Kiongozi huyo amesema Ukraine iko tayari kufanya mazungumzo ya amani na Urusi hata kuanzia kesho iwapo Moscow itaondoa wanajeshi wake ndani ya ardhi ya Ukraine.

Zelensky ameeleza kuwa, Rais wa Urusi Vladimir Putin hana nia ya kuvimaliza vita hivyo na inabidi azuiwe kwa njia yoyote ile - aidha ya kijeshi au kwa kutumia diplomasia.