1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Ulaya waelezea hisia zao juu ya Wafaransa kuikataa katiba ya Umoja wa Ulaya.

30 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CF8Z

Wakati huo huo viongozi wengine wa Umoja wa Ulaya,wameelezea hisia zao kufuatia matokeo hayo ya kura ya maoni juu ya katiba ya Umoja wa Ulaya iliyopigwa jana nchini Ufaransa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza,Jack Straw amesema matokeo hayo yanahitaji utulivu wa fikra juu ya mustakabali wa Umoja wa Ulaya.

Nae Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya,Jose Manuel Barroso amayaelezea matokeo hayo kuwa ni tatizo ambalo inabili litatuliwe.Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani,Joschka Fischer,amesema Wafaransa kuikataa katiba ya Umoja waUlaya ni jambo la kuhuzunisha na linauweka Umoja huo katika changamoto kubwa ya mustakabali wake.

Akizungumzia matokeo hayo Kansela wa Ujerumani,Gerhard Schröder,amesema kwa Wafaransa kutoiidhinisha katiba hiyo ni kikwazo,lakini hata hivyo hakitoweza kukwamisha hatma ya katiba hiyo kuweza kufanya kazi.