1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya mseto ya Ujerumani yaafikiana kuhusu bajeti

5 Julai 2024

Viongozi wa serikali ya mseto nchini Ujerumani inayoongozwa na vyama vitatu leo wamefikia makubaliano katika mazungumzo kuhusu bajeti ya taifa ya mwaka ujao 2025.

https://p.dw.com/p/4huD0
Ujerumani | Bajeti 2024 | Habeck, Scholz na Lindner wakiwa Berlin
Kansela Olaf Scholz(katikati) Waziri wa Uchumi Robert Habeck na Waziri wa Fedha, Christian Lindner katika picha ya pamoja mjini BerlinPicha: Florian Gaertner/photothek/IMAGO

Hayo yameripotiwa na shirika la habari la kijerumani la dpa,lililopata taarifa hizo kupitia vyanzo kadhaa vya serikali.

Viongozi hao pia wamefikia makubaliano ya awali kuhusu mpango wa bajeti utakaoimarisha ukuaji wa kiuchumi kwa zaidi ya asilimia 0.5 mwaka ujao.

Hatua ya kufikiwa makubaliano imekuja baada ya wiki kadhaa za mazungumzo kati ya Kansela Olaf Scholz, Waziri wa Uchumi ambaye ni naibu Kansela, Robert Habeck na Waziri wa Fedha Christian Lindner.

Bunge la Ujerumani linatarajiwa kuijadili rasimu hiyo ya bajeti kuanzia katikati ya mwezi Septemba na inaweza kupitishwa mwezi Novemba au Desemba.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW