1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Utawala wa kijeshi Niger wakutana na wajumbe kutoka Nigeria

10 Agosti 2023

Viongozi wa kijeshi nchini Niger wamekutana hapo jana na wajumbe wawili kutoka Nigeria, na hivyo kuleta matumaini ya kuwepo mazungumzo ya kukwamua mzozo wa kisiasa nchini humo.

https://p.dw.com/p/4Uzfl
Niger, Niamey | Mali und Burkina Faso demonstrieren Solidarität mit der Junta von Niger
Viongozi wa kijeshi wa Niger wakikutana na wanajeshi wa Burkina FasoPicha: RTN/Reuters

Wajumbe hao ni viongozi mashuhuri wa kimila ambao ni Lamido Muhammad Sanusi na Abdullsalami Abubakar.

Mazungumzo hayo yamefanyika huku Niger ikiishutumu Ufaransa kwa kukiuka anga yake na kushambulia kambi ya kijeshi na kuwaondoa kizuizini "magaidi" ili kuihujumu nchi hiyo.

Serikali ya Paris imekanusha tuhuma hizo.

Leo hii viongozi wa Jumuiya ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS wanatarajia kufanya mkutano wa kilele utakaoweza kuchukua hatua ya uingiliaji kijeshi ili kurejesha utawala wa kidemokrasia wa rais aliyepinduliwa madarakani Mohamed Bazoum.