1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa NATO kufanya mazungumzo na Rais Zelensky

11 Julai 2024

Viongozi wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO leo watafanya mazungumzo na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na kuelekeza mawazo yao kwenye changamoto kutoka China katika mkutano wa washirika wa Asia.

https://p.dw.com/p/4i9j3
Kiew NATO / Selenskyj und Stoltenberg
Picha: Ukrainian Presidency/abaca/picture alliance

Akizungumza pembezoni mwa mkutano wa NATO unaomalizika leo mjini Washington, Zelensky amewatolea wito washirika wa Ukraine hasa Marekani, kwenda mbali zaidi, ikiwemo kuvipa vikosi vyake vilivyozidiwa uwanja mpana zaidi wa kushambulia ndani ya Urusi.

Aidha, China imeionya NATO dhidi ya kuchochea mizozano katika uhusiano wake na Urusi. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Lin Jin, ameitaka NATO kutoupeleka mzozo sawa na huo barani Asia. 

Soma pia:NATO yashindwa kutoa mwaliko rasmi wa uanachama kwa Ukraine

Jana, viongozi wa NATO walitoa tamko la pamoja kuishutumu China kutokana na kuchukua jukumu muhimu la kuwa mwezeshaji mkuu wa Urusi katika vita vyake dhidi ya Ukraine.