1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Viongozi wa magharibi wakusanyika Kyiv kuonesha mshikamano

24 Februari 2024

Wakuu wa Mataifa manne ya Magharibi wamewasili mjini Kyiv hii leo kuonyesha mshikamano na Ukraine katika maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka miwili ya uvamizi kamili wa Urusi nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4cpVO
Volodymyr Zelensky, Ursula Von der Leyen na Alexander De Croo
Rais Volodomyr Zelensky akiwa pamoja na waziri mkuu wa Ubelgiji Alexander De Croo na Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, mjini Kyiv.Picha: picture alliance/dpa/Belga

Mawaziri wakuu wa Italia, Canada na Ubelgiji, ambao ni Giorgia Meloni, Justin Trudeau na Alexander De Croo jana usiku wamesafiri kwenda nchini humo pamoja na Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, wakitokea Poland kwa njia ya treni.

Von der Leyen aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba amekwenda Kyiv kusherehekea upinzani usio wa kawaida wa watu wa Ukraine na kuongeza kuwa wanasimama na Ukraine sasa kuliko wakati wowote ule hadi taifa hilo litakapokuwa huru.

Uwepo wa viongozi hao unaashiria kuonyesha msisitizo wa mataifa ya Magharibi kuendelea kuisaidia Ukraine hatakatika wakati inapokabiliwa na upungufu mkubwa wa silaha na kuathiri utendaji wake katika uwanja wa mapigano ambako Moscow inazidi kujinyakulia maeneo.