1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kusini

Yoon na Kishida wahofia ushirika wa Urusi na Korea Kaskazini

11 Julai 2024

Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol pamoja na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida wamezungumzia wasiwasi unaoletwa na ushirika unaoimarika kati ya Urusi na Korea Kaskazini na kukubaliana kuendeleza ushirikiano wa kijeshi.

https://p.dw.com/p/4i88G
Mkutano wa viongozi watatu nchini Korea Kusini
Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol akizungumza na viongozi wengine ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida(hawaonekani pichani) walipokutana kwenye mkutano mjini Seoul Mei 27, 2024Picha: JEON HEON-KYUN/Pool/REUTERS

Taarifa kutoka ofisi ya Yoon mapema leo imesema viongozi hao wawili wanaohudhuria mkutano wa kilele wa Jumuiya ya NATO, kwa mwaka wa tatu mfululizo, walikutana pembezoni na kujadiliana wasiwasi huo, mjini Washington siku ya Jumanne.

Tangu kuingia madarakani mwaka 2022, Yoon amejaribu kurekebisha uhusiano na Tokyo ulioathiriwa na mivutano ya kihistoria iliyoanzia na ukaliaji wa Japan nchini Korea kati ya mwaka 1910 hadi 1945. 

Seoul na Washington wamekuwa wakiishutumu Korea Kaskazini kwa kuipatia silaha Urusi inazotumia kuishambulia Ukraine.