1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSomalia

Viongozi wa kikanda wakubaliana kuiangamiza al-Shabab

2 Februari 2023

Viongozi wa Somalia, Djibouti, Ethiopia na Kenya wamekubaliana kupanga operesheni ya pamoja ya kijeshi ya ''kulisaka na kuliangamiza'' kundi la al-Shabaab ambalo linafanya mashambulizi kwenye ukanda huo.

https://p.dw.com/p/4N0QA
Gipfeltreffen der Frontstaaten Somalias in Mogadischu
Picha: Ethiopian PM Office

Viongozi wa Somalia, Djibouti, Ethiopia na Kenya wamekubaliana kupanga operesheni ya pamoja ya kijeshi ya ''kulisaka na kuliangamiza'' kundi la al-Shabaab ambalo linafanya mashambulizi kwenye ukanda huo.

Katika taarifa ya pamoja waliyoitoa jana kwenye mkutano wao wa kilele katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, viongozi hao wamesema operesheni hiyo itazuia harakati zozote za kundi hilo.

Viongozi hao wamekubaliana kufanya operesheni ya kulisambaratisha kundi hilo lenye itikadi kali za Kiislamu, kwenye maeneo ambayo bado yanakumbwa na mashambulizi ya kigaidi ili kuikomboa kabisa Somalia.

Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi wa mataifa yenye wanajeshi wake kwenye kikosi cha mpito cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia, ATMIS kinachohusika na operesheni dhidi ya wanamgambo.