1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Niger yadai kuzima jaribio la Bazoum kutaka kutoroka

Sylvia Mwehozi
20 Oktoba 2023

Msemaji wa watawala wa kijeshi Amadou Abduramane amedai kwamba Bazoum na familia yake, wapishi wake wawili na maafisa wawili wa usalama walijaribu kutoroka kutoka katika eneo wanakoshikiliwa.

https://p.dw.com/p/4XmLJ
Mohamed Bazoum
Rais aliyepinduliwa Niger Mohamed BazoumPicha: Evelyn Hockstein/Pool/File Photo/REUTERS

Viongozi wa kijeshi wa Niger wameeleza kuwa wamezima jaribio la rais aliyepinduliwa Mohamed Bazoum la kutaka kutoroka. Msemaji wa watawala wa kijeshi Amadou Abduramane amedai kwamba Bazoum na familia yake, wapishi wake wawili na maafisa wawili wa usalama walijaribu kutoroka kutoka katika eneo wanakoshikiliwa.Niger yamfukuza mratibu wa Umoja wa Mataifa

Abduramane ameongeza kwamba kiongozi huyo wa zamani alipanga kujificha nje ya mji mkuu wa Niamey kabla ya kuondoshwa kwa helkopita ya kigeni kuelekea Nigeria. Rais huyo wa zamani tangu alipoondolewa mamlakani mnamo Julai 26 amekataa kujiuzulu. Tangu wakati huo amekuwa akishikiliwa katika makaazi yake akiwa na mkewe na mtoto wao wa kiume. Mnamo mwezi Septemba mawakili wa rais huyo wa zamani waliwasilisha shauri katika mahakama ya jumuiya ya maendeleo ya kiuchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS dhidi ya wanajeshi waliompindua Bazoum.