1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Viongozi wa kijeshi Niger wamtangaza waziri mkuu mpya

8 Agosti 2023

Utawala wa kijeshi wa Niger umemteuwa waziri wa zamani wa uchumi, Ali Mahaman Lamine Zeine, kuwa waziri mkuu mpya. Tangazo hilo lililotolewa na baraza la kijeshi kupitia televisheni ya taifa.

https://p.dw.com/p/4UtFw
Ali Lamine Zeine
Ali Mahaman Lamine Zeine aliyechaguliwa kuwa waziri mkuu mpya wa NigerPicha: Matthew Cavanaugh/dpa/picture alliance

Utawala wa kijeshi wa Niger umemteuwa waziri wa zamani wa uchumi, Ali Mahaman Lamine Zeine, kuwa waziri mkuu mpya. Tangazo hilo lililotolewa usiku wa kuamkia leo na baraza la kijeshi kupitia televisheni ya taifa, limesema Lamine Zeine, ataapishwa kuanza kazi mara moja.

Mtaalamu huyo wa masuala ya kifedha, alihudumu kama waziri wa uchumi na fedha kwa miaka kadhaa chini ya rais wa wakati huo Mamadou Tandja, kabla ya kupinduliwa mwaka 2010. Katika siku za hivi karibuni, Lamine Zeine alikuwa akifanya kazi kama mchumi kwenye Benki ya Maendeleo ya Afrika nchini Chad.

Soma pia: Safari za ndege zatatizika kuelekea Afrika Magharibi

Hayo yakijiri, naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Victoria Nuland, amekutana hapo jana na kwa masaa mawili na viongozi wa kijeshi wa Niger kushinikiza kurejeshwa kwa serikali ya kiraia, lakini ameshindwa kupiga hatua yoyote. 

Ameyaelezea mazungumzo hayo kuwa ya kina na ukweli mtupu ingawa kuna wakati yalikuwa magumu. Nuland amesema aliwasilisha njia mbadala ambazo Marekani inataka zichukuliwe na kurejesha mahusiano ya pande hizo mbili. 

Hata hivyo, watawala wa kijeshi wa Niger hawakujibu ombi la naibu waziri huyo wa mambo ya kigeni wa Marekani kukutana na kiongozi mkuu wa kijeshi, Jenerali Abdourahamane Tiani wala rais aliyepinduliwa, Mohamed Bazoum. Jeshi la Niger lafunga anga

Hayo yakijiri, Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi, ECOWAS, imesema itafanya kikao siku ya Alhamis kuamua hatua zinazofuata baada ya utawala wa kijeshi wa Niger kukataa kutekeleza matakwa ya kumuachia huru na kumrejesha madarakani Bazoum ambaye ni mshirika mkubwa wa mataifa ya Magharibi.