1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJapan

Viongozi wa G7 watilia shaka China kuunda silaha za nyuklia

19 Mei 2023

Kundi la nchi saba tajiri duniani G7 limesema baada ya mazungumzo yao juu ya silaha za nyuklia, kwamba ongezeko la China kutengeneza silaha hizo linatia wasiwasi kwa usalama na utulivu wa dunia na kikanda.

https://p.dw.com/p/4RahW
Viongozi wa Kundi la G7 wanaokutana nchini Japan
Viongozi wa Kundi la G7 wanaokutana nchini JapanPicha: Jacques Witt/Pool/AFP

Katika taarifa yao ya pamoja kundi hilo limesema, hatua ya China ya kuzidi kutengeneza silaha hizo kwa usiri inaleta wasiwasi wa kiusalama na kusisitiza haja ya kusitisha biashara na taifa hilo.

Wakati huo huo, viongozi hao wa nchi hizo 7 tajiri duniani wamekubaliana kuiwekea Urusi vikwazo zaidi huku taarifa rasmi ya kundi hilo ikisubiriwa kutolewa mwishoni mwa mkutano huo mjini Hiroshima Japan.

Mataifa hayo yamekubaliana kusitisha usafirishaji wa bidhaa nchini Urusi unaoweza kuisaidia katika vita vyake vya miezi 15 nchini Ukraine.