1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAfrika

Viongozi wa dini Tanzania kupigia chapuo chanjo ya Covid-19

Hawa Bihoga28 Julai 2021

Baadhi ya viongozi wa dini nchini Tanzania wamesema watabeba jukumu la kueleza umuhimu wa chanjo ya Covid-19 katika dunia ya sasa inayokabiliwa na janga hilo hatari lililogharimu masiaha ya mamilioni ya watu ulimwenguni.

https://p.dw.com/p/3yCWT
Tansania Dar es Salaam | Kassim Majaliwa
Picha: Tanzania Presidents Office

Kauli za wale wanaoipinga chanjo zinanadi kuwa, chanjo hiyo inabadili mfumo wa vinasaba vya mtu jambo ambalo limekatazwa katika baadhi ya iman za dini, lakini hoja za wengine zisizojiegemeza kwenye imani zinasema huu ni mpango wa mataifa tajiri katika kupunguza idadi ya watu ulimwenguni, jambo ambalo limepingwa vikali kupitia machapisho ya kisayansi na maandiko ya kidini.

Kauli za baadhi ya viongozi wa dini zinaonesha imani kubwa iliojaa ushawishi na utayari kwamba watainadi chanjo kwani ni sehemu ya tiba ambayo imethibitishwa na wanasayansi katika kukabiliana na janga la corona ambalo limegharimu maisha ya watu zaidi ya milioni tatu ulimwenguni na kuyaacha mataifa yakiwa kwenye tafakuri pana katika kujinasua kwenye janga hilo.

Soma pia: Hatua ya Samia kuhusu Covid ni ya kupongeza

Tansanina | COVID-19 Impfstoff aus der COVAX Initiative
Waziri wa afya wa Tanzania Dorthy Gwajima, waziri wa mambo ya nje Balozi Liberata Mulamula, na balozi wa Marekani nchini Tanzania Donald Wright wakiwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar es Salaam kupokea shehena ya kwanza ya chanjo ya covid-19, Julai 24, 2021, iliyotolewa na Marekani.Picha: Domasa Sylivester/AP/picture alliance

Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Aboubakari Bin Zuber amesema Waislamu wanaotaka kwenda hija ya umra watalazimika kupata chanjo, hivyo ni muhimu huku mwenzake Askofu Thadeus Ruwaichi mkuu wa jimbo kuu la Dar es salaam akiwaambia wanahabari kuwa, watu waondoe hofu kwani tayari wanasayansi wameithibitisha ni salama kwa binadamu na hata kuwataka wengine kujielimisha zaidi.

Ingawaje dozi za chanjo hiyo zipatazo milioni moja elfu hamsini na nane mia nne tayari zipo nchini, lakini bado kumetawala ajenda ya kudhoofisha mpango wa serikali wa utolewaji chanjo wa hiari kwa watu wake.

Anthony Lusekelo kiongozi wa kidini alie na ushawishi mkubwa, amesema yupo tayari kubeba jukumu la kueleza waumini wake juu ya umuhimu wa chanjo hiyo, kwani hakuna kiongozi alie tayari kulitoa taifa lake kwa ajili ya maslahi yake binafsi au ya wengine.

Soma pia: Tanzania yasitisha safari za kuelekea India

Tayari wizara ya afya nchini humo imesema kuanzia Jumatano chanjo zimeanza kusambazwa katika maeneo mengine ya nchi na hadi kufikia mapema mwezi ujao mikoa yote itakuwa imepata chanjo hiyo.

Taifa hilo la Afrika Mashariki ambapo awali ilionesha kutokubali mpango wa chanjo, limesema litaendelea kuruhusu chanjo zingine za aina mbalimbalo ikiwemo Sinovac, Johnson Johnson pamoja na Pfizer baada ya kujiridhisha juu ya usalama wake.