1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Afrika walaani mashambulizi ya Israel huko Gaza

Hawa Bihoga
17 Februari 2024

Viongozi katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika unaofanyika mjini Addis Ababa Ethiopia, wamelaani kile walichokiita "hujuma ya Israel" katika Ukanda wa Gaza na kutaka kukomeshwa mara moja.

https://p.dw.com/p/4cWpZ
Ethiopia | Mkutano wa AU mjini Addis Ababa
Ukumbi wa mikutano kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa.Picha: Solomon Muchie/DW

Katika ufunguzi wa mkutano huo Rais wa Halmashauri ya Kuu ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat amesema, mashambulizi ya Israel ni "ukiukwaji wa wazi" wa sheria za kimataifa za kibinadamu na kuishutumu Israel kwa "kuwaangamiza" wakaazi wa Gaza.

Faki alimuhakikishia Waziri Mkuu wa mamlaka ya ndani ya Palestina Mohammad Shtayyeh ambae amehudhuria mkutano huo kuwa wanaonesha mshikamano na watu wa Palestina kutokana na kile alichokisema "mashambulizi ambayo hayajawahi kutokea katika historia ya wanadamu."

Aidha Faki amezungumzia wasiwasi wa kuzuka upya kwa mapinduzi ya kijeshi barani humo, huku akigusia mizozo ikiwemo mkwamo wa kisiasa nchini Senegala, ghasia mashiri mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Ametoa wito wa mshikamano ili kukabiliana na changamoto katika bara hilo lenye watu takriban bilioni 1.3.