1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kilele wa AU wagubikwa na mizozo na mapinduzi

Hawa Bihoga
17 Februari 2024

Viongozi wa Afrika wanakusanyika mjini Addis Ababa kwa mkutano wa klele wa siku mbili leo,chini ya kiwingu cha mapinduzi ya kijeshi yaliyoshuhudiwa kwenye mataifa ya bara hilo ambalo pia linapambana na mizozo

https://p.dw.com/p/4cWEc
Addis Ababa, Ethiopa | viongozi wa Afrika katika picha ya pamoja
Viongozi wa Umoja wa Afrika wakiwa katika picha ya pamoja mjini Addis AbabaPicha: Eduardo Soteras/AFP/Getty Images

Awali kabla ya mkutano huo wa Kilele mjini Addis Ababa Ethiopia, Rais wa Halmashauri ya Kuu ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat alitahadharisha juu ya ghasia zinazoyakumba mataifa ya Afrika, akiutaja mzozo wa muda mrefu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kitisho cha wanamgambo wa itikadi kali nchini Somalia, hatari ya ugaidi kwenye kanda ya Sahel na ukosefu wa utulivu nchini Libya.

Kando na mkutano huo mkuu wa kilele wa Umoja wa Afrka, kulifunguliwa mkutano mdongo unaolenga kufufua upya mchakato wa amani nchini Kongo uliofanyika hapo jana Ijumaa.

Soma pia:DRC: Mkutano wa AU walenga kuinua sauti ya Afrika kwenye jukwaa la kimataifa

Katika mkutano huo wa kilele mataifa ya Gabon na Niger hayatahudhuria kutokana na kusimamishwa uanachama kufuatia mapinduzi ya kijeshi, yakiungana na Mali, Guinea, Sudan na Burkina Faso ambazo pia zilipigwa marufuku.