1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMali

Viongozi wa Afrika Magharibi kujadili usalama nchini Mali

19 Julai 2023

Viongozi kadhaa wa Afrika Magharibi wamekutana Nigeria kujadili njia za kuhakikisha usalama nchini Mali, baada ya kufika mwisho kwa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo.

https://p.dw.com/p/4U6eY
Viongozi wa Afrika Magharibi wanaowajumuisha rais wa Nigeria President Muhammadu na rais wa Guinea Bissau Umaro Sissoco Embalo wakihudhuria hafla ya kuanza ujenzi wa makao makuu ya Ecowas mjini Nigeria mnamo Desemba 4, 2022
Baadhi ya viongozi wa Afrika MagharibiPicha: Afolabi Sotunde/REUTERS

Viongozi hao ambao ni marais wa Nigeria Bola Tinubu pamoja na wenzake wa Niger, Guinea-Bissau na Benin, pia wanajadiliana kuhusu kuirudisha Mali katika demokrasia baada ya mkururo wa mapinduzi. Wanachama watatu wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS Mali, Burkina Faso na Guinea ni nchi zinazoongozwa kijeshi baada ya mapinduzi mara tano miongoni mwao tangu mwaka 2020. Makundi ya kigaidi ya Al-Qaeda na lile linalojiita Dola la Kiislamu, yanazidi kuenea katika eneo la Sahel na sasa yanapeleka machafuko kusini katika pwani ya mataifa ya Afrika Magharibi.