1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ECOWAS: Juhudi za kukomesha mapinduzi hazijazaa matunda

10 Desemba 2023

Viongozi wa Mataifa ya Afrika Mgharibi wanakutaka mjini Abuja Nigeria, kuendelea kushinikiza kuheshimiwa kwa demokrasia katika mataifa yanayotawaliwa kijeshi.

https://p.dw.com/p/4ZzWE
Mkutano wa ECOWAS Ghana
Moja ya mikutano wa viongozi wa Jumuiya ya kiuchumi ya ECOWASPicha: Richard Eshun Nanaresh/AP/dpa/picture alliance

Viongozi wa Mataifa ya Afrika Mgharibi wanakutaka mjini Abuja Nigeria, kuendelea kushinikiza kuheshimiwa kwa demokrasia katika mataifa yanayotawaliwa kijeshi. Viongozi hao kwa mara ya kwanza wametambua kuwa juhudi zao za kukomesha wimbi la mapinduzi hazijafanikiwa.

Viongozi hao nchi 15 wanachama wa Jumuiya ya kiuchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS hawajafanikiwa kurejesha uthabiti wa kisiasa katika kanda nzima ya kati na Magharibi mwa Afrika zilizorekodi mapinduzi mara 8 tangu mwaka 2020 ikiwa ni pamoja na Niger na Gabon.

Soma zaidi: Viongozi wa ECOWAS wakutana kujadili muelekeo wa mataifa yaliyo chini ya utawala wa kijeshi

Mwezi uliopita serikali ya Sierra Leone na Guinea-Bissau pia zilielezea kupitia migogoro ya kisiasa kufuatia majaribio ya mapinduzi.

Omar Alieu Touray, rais wa kamisheni ya ECOWAS  ameuambia mkutano huo hii leo kwamba licha ya vikwazo na juhudi nyengine za kujaribu kurejesha utawala wa kiraia katika mataifa yaliyokumbwa na mapinduzi, Jeshi limeendelea kuitawala Niger huku utawala wa kijeshi pia nchini Mali na Burkina Faso zikiacha kushirikiana na kamisheni hiyo kuhusu mataifa yao kurejea katika utawala wa kiraia.