1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ECOWAS yawaonya wagombea urais Liberia

16 Oktoba 2023

Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) imewataka wagombea wa uchaguzi nchini Liberia kujiepusha na kutangaza ushindi kabla ya wakati au kuweka shinikizo lisilofaa kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

https://p.dw.com/p/4XZnK
Liberia Wahl 2023
Picha: John Wessels/AFP

ECOWAS imesema itakabiliana na wachochezi wa ghasia huku ikiwapongeza watu wa Liberia kwa mchakato wa amani wa upigaji kura na kuwataka waendelee kuwa wavumilivu wakati wakisubiri matokeo.

Jumuiya hiyo imewataka wadau wote kutii kanuni za kidemokrasia.

Soma zaidi: Waangalizi wa kimataifa waipongeza Liberia kwa uchaguzi wake

Raia wa Liberia walipiga kura Oktoba 10 na kuamua iwapo watamchagua tena gwiji wa soka George Weah kwa muhula wa pili kama rais, pamoja na kufanya uchaguzi wa Bunge.

Kwa sasa kura zinaendelea kuhesabiwa na matokeo ya mwisho yatatangazwa ndani ya wiki mbili baada ya uchaguzi.